Hii ni habari njema kwa Wananchi baada ya uongozi wa klabu ya Yanga kufanikiwa kumuongezea mkataba wa miaka miwili mlinzi wa kulia Kibwana Shomari
Kulikuwa na tetesi nyingi kuhusu Kibwana ambapo zipo taarifa za hakika kuwa Simba walijaribu kumshawishi kupitia watu wake wa karibu ajiunge nao
Kibwana amethibitisha kuwa tayari ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumikia Yanga
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema wanaendelea na mchakato wa kuwaongezea mikataba wachezaji wote ambao kocha Nasreddine Nabi amewahitaji kuendelea nao msimu ujao
ADVERTISE HERE