Msemaji wa klabu ya Yanga Haji Manara amewataka Wanachama na Mashabiki wa timu hiyo kuwa na utulivu hasa baada ya matokeo ya suluhu ya bila kufungana dhidi ya Prisons hapo jana
Ulikuwa mchezo wa tatu mfululizo Yanga inashindwa kupata ushindi ikiwa ni pamoja na kutofunga bao lolote
Manara amesema matokeo hayo hakuna aliyeyatarajia kuanzia kwa viongozi, benchi la ufundi, wachezaji na hata mashabiki ambao wameibua mijadala mingi kwenye kurasa za mitandao ya kijamii
Amesema hakuna mechi ambayo Yanga imecheza vizuri na kutengeneza nafasi kama mchezo wa jana dhidi ya Prisons lakini walikosa bahati tu ya kutumbukiza mpira wavuni
ADVERTISE HERE