Baada ya Msemaji wa Yanga Haji Manara kuweka 'post' kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii akimwagia sifa winga wa Simba Bernard Morrison, tetesi zimeshika kasi kumuhusisha winga huyo na kurejea Yanga
Morrison ni mchezaji ambaye haishiwi vituo, ni wiki iliyopita tu alimchoma 'bisibisi' shabiki wa Yanga baada ya kichukizwa na utani aliokumbana nao baada ya mchezo wa watani wa jadi
Ni mchezaji ambaye alifanikiwa sana wakati yuko Yanga, miezi sita aliyowatumikia Wananchi ilikuwa bora sana lakini akahadaika na Simba, akaukana mkataba wa Yanga
Mapungufu ya mkataba aliosaini na Yanga yakapelekea ashinde rufaa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS)
Kwa mfululizo wa matukio yaliyotokea kati yake na Yanga, haitakuwa rahisi kwake kusajiliwa tena na Yanga
Imeelezwa mkataba wake na Simba uko ukingoni na mwenyewe anatamani kurejea tena kwa Wananchi