Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesisitiza kuwa hakufanya kose lolote katika mchezo wa kombe la FA dhidi ya Geita Gold hadi kupelekea akapewa kadi nyekundu iliyomfanya akose michezo mitatu iliyopita
Nabi amabaye amemaliza adhabu hiyo, amesema katika maisha yake ya ukufunzi wa soka hakuwahi kuonyeshwa kadi nyekundu kwa makosa ya utovu wa nidhamu
"Napenda nilizungumze hili kwani lilinikwaza sana. Nimeona taarifa waamuzi inabainisha kuwa nilipewa kadi nyekundu kwenye mchezo dhidi ya Geita Gold baada ya kuwatukana waamuzi"
"Ukweli sikutenda kosa hilo, naona ni dhurma imefanyika kwangu na klabu ya Yanga. Mimi sijawahi kupewa kadi nyekundu katika maisha yangu ya ukufunzi wa soka, sikutukana na ni kawaida yangu kila baada ya mchezo nawasilimu waamuzi," alisema Nabi
Akizungumzia maandalizi kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons ambao utapigwa kesho Jumatatu katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Nabi amesema wako tayari kwa mchezo huo, morali ya wachezaji iko juu wanafahamu wanahitaji kushinda
"Wachezaji wote wako tayari, morali yao iko juu wanafahamu tunahitaji kushinda baada ya kutopata ushindi katika michezo miwili iliyopita"