Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema wamejiandaa kikamilifu kuikabili Tanzania Prisons katika mchezo wa ligi kuu ya NBC ambao utapigwa kesho Jumatatu katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Baada ya kuambulia alama mbili kati ya sita katika michezo miwili iliyopita, Bumbuli amesema Yanga imedhamiria kutumia vyema uwanja wake wa nyumbani licha ya kutambua ugumu wa mchezo huo
"Tunarejea katika uwanja wa nyumbani kupambana dhidi ya Tanzania Prisons, tunafahamu hata wao hawana matokeo mazuri na wanahitaji kujikwamua kutoka pale walipo"
"Lakini na sisi tunahitaji kushinda ili kuzidi kuongeza wigo wa alama dhidi ya wanaotufuata katika mbio za kuwania ubingwa"
"Tunawaomba mashabiki wetu waje kwa wingi uwanjani kuwashangilia wachezaji wao, huu ni mchezo ambao tunahitaji kushinda," alisema Bumbuli