Mshambuliaji wa Geita Gold George Mpole jana alifunga bao lake la 12 msimu huu na kumfikia Fiston Mayele wa Yanga
Wawili hao wameingia katika ushindani wa aina yake katika vita ya kuwania ufungaji bora
Baada ya kutofunga katika michezo miwili iliyopita, Mayele atakuwa na shauku kubwa ya kufunga katika mchezo dhidi ya Tanzania Prisons ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa kesho
Pamoja na kufunga mabao 12, Mayele na Mpole wote wametoa pasi tatu za mabao
Reliants Lusajo wa Namungo Fc yuko nafasi ya tatu akiwa amefunga mabao 10 na kutoa pasi nne za mabao
ADVERTISE HERE