Beki wa klabu ya Yanga Dickson Job amesema wachezaji wote hawapo tayari kuona wanapoteza mchezo kwani lengo lao ni kumaliza Ligi pasipo kupoteza mchezo
Yanga mpaka sasa wamecheza mechi 22 bila kupoteza na kuifanya iwe timu pekee yenye rekodi hiyo kwenye Ligi Kuu ya NBC msimu huu
Job amesema ili wakamilishe lengo hilo, wanahitaji kucheza mechi bila kuruhusu goli huku kila mchezaji akipambana kuhakikisha wanafanikiwa
Job amezungumzia 'pacha' yake na nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto ambapo amesema kucheza kwao pamoja kwa muda mrefu ndio siri ya ubora wao kwenye safu ya ulinzi ya Yanga
"Mimi na Mwamnyeto tuna maelewano makubwa na kucheza kwetu muda mrefu tunajuana vizuri na ndio maana kila mmoja anatoa kile anachostahili kwa wakati," alisema Job
Job na Mwamnyeto wamekuwa nguzo muhimu ya safu ya ulinzi ya Yanga, nyota hao pia wakiwa tegemeo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania kinachonolewa na kocha Kim Poulsen