Licha ya kutofunga katika michezo miwili iliyopita dhidi ya Simba na Ruvu Shooting, mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele bado anaongoza mbio za kuwania kiatu cha dhahabu akiwa na mabao 12
Mshambuliaji wa Geita Gold George Mpole amesogea mpaka nafasi ya pili baada ya kufikisha mabao 11 huku nafasi ya tatu ikishikiliwa na Reliants Lusajo ambaye naye hajafunga katika mechi kadhaa zilizopita
Mayele amekuwa akikamiwa na walinzi wa timu pinzani kutokana na makali yake, amesema ataendelea kutetema kwenye michezo ijayo

"Sijafunga katika michezo miwili iliyopita, sijafurahi kwa sababu siku zote mimi napenda kufunga niisaidie timu yangu na kuwafurahisha mashabiki. Kila tunapocheza mashabii wetu wanasubiri kutetema hivyo nitaendelea kupambana kwenye michezo ijayo kuhakikisha wanatetema," alisema Mayele
Mayele anafukuzia rekodi za aina mbili, akiwa na michezo nane kukamilisha rekodi hizo
Kwanza ni kuvunja rekodi ya mabao 14 aliyofungwa kwenye ligi kuu ya DR Congo msimu uliopita akiwa na AS Vita ambapo alimaliza katika nafasi ya pili kwenye orodha ya wafungaji bora
Lakini pia Mayele amejiwekea malengo ya kuibuka kuwa mfungaji bora wa ligi kuu ya NBC msimu huu