Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amemaliza adhabu ya kukosa michezo mitatu kutokana na kadi nyekundu aliyopewa kwenye mchezo wa kombe la FA dhidi ya Geita Gold
Mchezo dhidi ya Ruvu Shooting ni wa tatu Nabi kukosekana kwenye benchi la ufundi pia akikosa michezo dhidi ya Namungo Fc na Simba
Hii ni habari njema kwa Yanga kuelekea mchezo dhidi ya Tanzania Prisons ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa May 09
Baada ya kudondosha alama mbili leo mkoani Kigoma, Yanga inahitaji ushindi katika mchezo dhidi ya Prisons kuendelea kuukaribia ubingwa
ADVERTISE HERE