Kimahesabu Yanga inahitaji kushinda angalau michezo mitano kujihakikishia ubingwa wa ligi kuu msimu huu ambao utakuwa ubingwa wao wa 28 katika historia
Wakicheza katika uwanja wa Lake Tanganyika dhidi ya Ruvu Shooting, matokeo ya ushindi yatawafanya Wananchi wasogee karibu ya ubingwa kwani watabaki na michezo minne ya kutangaza ubingwa
Ndio maana mchezo dhidi ya Ruvu Shooting ni kama fainali kwa Yanga
Jana alipozungumza kwenye Mkutano na Wanahabari kuelekea mchezo huo, Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze alisema leo watatumia wachezaji bora 11 katika kila nafasi
Kwa maana Ruvu Shooting watarajie kukutana na kikosi bora zaidi cha Yanga
Katika mchezo huo ni wachezaji wawili tu ambao watakosekana, Yacouba Songne anayeendelea kuimarika na Chico Ushindi aliyeachwa jijini Dar es salaam licha ya kuwa amepona maradhi yaliyomfanya akose mchezo uliopita dhidi ya Simba
Kocha Mkuu Nasreddine Nabi ataendelea kubaki jukwaa katika mchezo wa tatu ambao ni wa mwisho kukamilisha adhabu ya kadi nyekundu