Kikosi cha Yanga kiliwasili mkoani Kigoma jana kuelekea mchezo wao wa ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting ambao utapigwa kesho Jumatano kunako uwanja wa Lake Tanganyika
Ni sikukuu ya Eid ambapo Waislam wa Tanzania na wenzao kote dunia wanasherehekea sikukuu hii baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan
Wachezaji, benchi la ufundi na viongozi ambao wako kwenye msafara wa Yanga uliotua Kigoma, wao wanasherehekea sikukuu pamoja
Jioni ya leo Yanga itakamilisha maandalizi yao ya mwisho katika uwanja wa Lake Tanganyika tayari kuwakabili Ruvu Shooting
Mkakati wa Wananchi ni kuhakikisha wanashinda michezo mitano inayofuata wakianza na Ruvu Shooting ili kujihakikishia ubingwa mapema
ADVERTISE HERE