Juzi katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba, Yanga iliweka rekodi ya mapato katika mechi zote za mashindano zilizopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa msimu huu
Msemaji wa Yanga Haji Manara amebainisha kuwa mchezo huo ambao Yanga ilikuwa mwenyeji, uliingiza takribani Tsh 320m
Mchezo wa duru ya kwanza ambao Simba alikuwa mwenyeji uliingiza Tsh 257m
Aidha mchezo wa kombe la Shirikisho kati ya Simba dhidi ya Orlando pirates ambao ulikuwa ukitajwa kuingiza mashabiki wengi, mapato yaliyopatikana ni Tsh 197m
Manara amewapongeza mashabiki wa Yanga kwa kuthibitisha ukubwa wao kwa vitendo na sio maneno kama wafanyavyo wengine
"Kama huna takwimu, huna haki ya kuzungumza, sisi tunatamba ukubwa wetu kulingana na takwimu," alisema Manara
ADVERTISE HERE