Yanga chupuchupu Mbeya, yapita kiume kombe la FA

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
31 Jan 2018
Yanga chupuchupu Mbeya, yapita kiume kombe la FA
Mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga wamesonga mbele michuano ya kombe la FA baada ya kushinda kwa mikwaju ya penati 4-3 kufuatia sare ya bao 1-1 dhidi ya Ihefu FC.

Bao la Ihefu FC lilikuwa la kujifunga baada mpira wa chini kumshinda mlinda lango Youthe Rostand kisha kumgonga beki Andrew Vicent na kutumbukia wavuni.

Pengine mazingira ya uwanja yalipelekea mpira huo kubadili mwelekeo kabla ya kumpoteza kipa Rostand.

Yanga ilikosa nafasi kadhaa za wazi kupitia kwa washambuliaji wake Obrey Chirwa na Amissi Tambwe aliyekosa bao la wazi kwenye dakika ya kwanza ya mchezo.

Kipindi cha pili Yanga ilitumia muda mwingi langoni mwa Ihefu lakini mlinda lango Andrew Kayuni alikuwa kikwazo kikubwa.

Yanga ilisawazisha dakika za majeruhi kupitia mkwaju wa penati uliopigwa na Obrey Chirwa kwenye dakika za lala salama kabisa baada ya yeye mwenyewe kufanyiwa madhambi.

Yanga ikaweza kusahihisha makosa yake kwenye mikwaju ya penati na kuibuka na ushindi wa penati 3-4

Kelvin Yondani, Hassani Kessy, Raphael Daudi na Gadiel Michael walifunga penati nne za Yanga huku Tshishimbi na Chirwa wakikosa mikwaju yao.

Youthe Rostand alikuwa shujaa wa Yanga baada kuikoa timu yake kwenye mikwaju ya penati

Vijana wa Ihefu FC walionyesha upinzani mkali kwa Yanga, wanastahili pongezi kwa upiganaji wao lakini uzoefu umeipa mafanikio Yanga siku ya leo

Vigogo wengine Azam FC wamesonga mbele kibabe baada ya kuichapa Shupavu FC ya mkoani Morogoro kwa mabao 5-0

Matokeo ya michezo yote
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’