Ni Matchday; Yanga vs Simba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Apr 2022
Ni Matchday; Yanga vs Simba

Hatimaye ile siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini imewadia

Mchezo namba moja kwa ukubwa katika ligi kuu ya NBC, Yanga dhidi ya Simba unapigwa leo katika uwanja wa Benjamin Mkapa, kuanzia saa 11 jioni

Ni mchezo wa hesabu kwa makocha wa timu zote mbili, kocha Nasreddine Nabi wa Yanga anafahamu kama kikosi chake kitaibuka na ushindi kitajiweka katika nafasi nzuri sana ya kushinda ubingwa kwani watakuwa juu ya msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama 16 dhidi ya wapinzani wao Simba

Kocha Pablo Franco wa Simba ametoka kuondoshwa kwenye michuano ya kombe la Shirikisho hatua ya robo fainali kule Afrika Kusini

Ni mchezo ambao unaweza kutoa taswira ya vile wanakwenda kuhitimisha msimu huu

Kama watapoteza mchezo, yale matumaini madogo ya kutetea ubingwa ni wazi watayapoteza na zaidi watalazimika kujikita katika kujihakikishia nafasi ya pili

Lakini pia ni kama hatma ya Pablo iko mikononi mwa mchezo huu, kipigo kutoka kwa Wananchi kitamuweka katika hatari ya kuonyeshwa mlango wa kutokea

Pamoja na kuingia katika mchezo huo wakiwa na mtaji mkubwa wa pointi, Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema watawaheshimu wapinzania wao na kuwa hawafikirii idadi ya pointi walizonazo kwani wanafahamu katika mchezo wowote wa dabi, takwimu hazikupi uhalali wa kushinda

Amesema Yanga itacheza mpira wake wa siku zote, pasi na mikimbio mingi, lakini watachukua tahadhari kwani wapinzani wao nao wana timu nzuri

Pablo yeye ametamba kuwa wana kikosi bora kuliko Yanga na haoni kama mchezo wa leo utakuwa mgumu kwa upande wao

Mwisho wa siku dakika 90 zitaamua nani atalia na nani ataondoka na kicheko!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
10h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’