Msemaji wa klabu ya Yanga Haji Manara amewahakikishia wachezaji kuwa siku ya kesho watapata uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa washabiki wao katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba
Manara amesema uongozi, Wadhamini, GSM wametimiza wajibu kuhakikisha wanawawekea mazingira mazuri kuelekea mchezo huo
Sasa ni jukumu lao kuwapa furaha Wananchi ambao msimu huu hawana kingine wanachohitaji zaidi ya ubingwa wa ligi kuu
Manara amewapa ujumbe huu wachezaji wa Yanga;
"Uongozi ushatimiza kinachotakiwa kufanywa, Uwanjani ni wazi Washabiki wetu watakuwa wengi zaidi ya wa kwao
Kwa vyovyote vile, GSM atafanya yake kuelekea mechi ya kesho. Sasa ni zamu yenu Wachezaji wetu kwenda kutupa furaha Wananchi.
Nendeni mkacheze bila Presha, mkacheze mchezo wenu ule ule wa pasi nyingi na kuwafungua wapinzani uwanjani,
Nendeni mkawapress, huku mkicheza kwa nidhamu kubwa ya kuwaheshimu wapinzani wenu bila kuwaogopa.
Katimizeni wajibu wenu ambao Wananchi washaufanya kwenu, kawaonyesheni Wanayanga dhamira yenu ya kushinda game hii na ubingwa huu kwa vitendo.
Mnao ubora mkubwa na tayari mshathibitisha hilo Kwa mechi zote ishirini za ligi kuu mlizokwisha cheza hadi sasa, takwimu za huo ubora zipo side yenu
Nyinyi ni wajuzi mno na mna uzoefu mkubwa wa mitanange kama hii, tunawapenda na tunajua uwezo wa kutupa amani kesho mnao. Wekeni dhamira ya kushinda kesho na Insha'Allah Mungu atakuwa nanyi"
TUNAWAAMINI