Waziri wa TAMISEMI Mhe. Innocent Bashungwa atakuwa mgeni rasmi wa mechi ya mkondo wa pili wa ligi kuu Tanzania bara kati ya Yanga hidi ya Simba utakaopigwa Jumamosi Aprili 30, 2022 katika dimba la Benjamin Mkapa
Mtanange huo wa kukata na shoka, utapigwa kuanzia saa 11 jioni
Wakiwa kileleni mwa msimamo wa ligi na alama zao 54, Wananchi wamepania kwelikweli kuongeza alama nyingine tatu mbele ya Waziri Bashungwa na kuendelea kuukaribia ubingwa wa ligi kuu msimu huu
ADVERTISE HERE