Ndivyo unavyoweza kusema kutokana na kazi nzuri inayofanywa na mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele
Wapo watu wanajaribu kufifisha makali ya Mayele kwa kauli zao kusema ni mshambuliaji wa kawaida
Alianza Afisa Habari wa Azam Fc Thabit Zacharia, akafuata kocha msaidizi wa Namungo Fc Jamhuri Kiwhelo ingawa jana baada ya mchezo dhidi ya Namungo Fc, Julio alifuta kauli yake na kukubali kuwa Mayele ni mshambuliaji hatari
Hapa tunamzungumzia mshambuliaji ambaye amefunga katika michezo sita mfululizo kwenye ligi kuu ya NBC
Aliwafunga Mtibwa Sugar, Kagera Sugar, Geita Gold, KMC, Azam FC na Namungo FC hapo jana akifikisha mabao 12
Ni mshambuliaji ambaye amedhihirisha kuwa hazuiliki, itoshe kusema kwa sasa Mayele ndiye mshambuliaji bora kwenye ligi kuu ya NBC
Aliahidi kuwa atafunga mchezo dhidi ya Namungo Fc jana, akafunga lakini pia alitoa ahadi atafunga katika mchezo unaofuata kwenye ligi dhidi ya Simba, bila shaka atafunga!