Mapema leo wakati akizungumza na wanahabari, kocha msaidizi wa Yanga Cedric Kaze alisema viungo Khalid Aucho na Feisal Salum 'Fei Toto' wamerejea kikosini baada ya kupona majeraha yao
Wachezaji hao wanaweza kuwa sehemu ya kikosi kitakachoshuka uwanjani kuikabili Namungo Fc hapo kesho, mchezo ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Kocha Nasreddine Nabi atajiridhisha na utimamu wao kwenye mazoezi ya mwisho leo, anaweza kuwatumia wote katika mchezo huo
Kaze alisema hawatafanya 'rotation' yoyote ya kikosi kwani alama tatu za mchezo wa Namungo Fc ni muhimu sana
ADVERTISE HERE