Yanga vs Namungo Fc, ni Jumamosi hii

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Apr 2022
Yanga vs Namungo Fc, ni Jumamosi hii

Baada ya kukosa burudani ya timu yao kwa timu yao kwa takribani siku 10, burudani inarejea kwa mashabiki wa Yanga kesho Jumamosi April 23 wakati wananchi watakaposhuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Namungo Fc katika mchezo wa ligi kuu ya NBC

Huu ni mchezo muhimu sana kwa Yanga katika kampeni yao ya kuwania ubingwa wa ligi kuu msimu huu

Ushindi utawafanya Yanga waendelee kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi kwa alama nyingi zaidi kabla ya mchezo dhidi ya watani zao Simba ambao utapigwa April 30

Kama Yanga itapata ushindi dhidi ya Namungo Fc halafu ikashinda mchezo unaofuata dhidi ya Simba, itafikisha alama 57, alama 16 zaidi dhidi ya timu itakayokuwa inafuata kwenye nafasi ya pili katika msimamo wa ligi

Lakini muhimu zaidi ni kuwa Yanga inatumia mchezo huu kama sehemu ya maandalizi kuelekea mchezo dhidi ya Simba April 30

Ratiba ya awali ilikuwa ikionyesha Yanga isingecheza mchezo wowote wa ligi mpaka April 30 watakapoikabili Simba

Hata hivyo ratiba hii ilikuwa imekaa 'kimtego' sana kwani wachezaji wangekaa takribani wiki tatu pasipo kucheza mechi

Ni kipimo sahihi kwa Yanga kuelekea mchezo huo muhimu ambao unaweza kuihakikishia Yanga ubingwa msimu huu

Namungo Fc imekuwa ikiwapa wakati mgumu Wananchi katika michezo wanayokutana. Tangu walipopanda daraja misimu mitatu iliyopita, si wao wala Yanga waliowahi kupata ushindi kwenye mchezo wa ligi

Hivyo Wananchi wataingia katika mchezo huu wakiwa na shauku ya kutaka 'kuvunja mwiko' wa kukosa ushindi dhidi ya Namungo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
2h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
6h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
10h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
11h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
14h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’