Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema takwimu za michezo iliyopita kati ya Yanga dhidi ya Namungo Fc, zinaufanya mchezo wa Jumamosi kuwa na umuhimu mkubwa
Nabi amesema Jumamosi wanakutana na timu nzuri ambayo imekuwa ikiwapa wakati mgumu kila wanapokutana kwenye ligi
Nabi amesema mechi hiyo itakayopigwa Aprili 23 ina uzito mkubwa katika mbio za ubingwa, pia itasaidia kuwapa morali nzuri kabla ya kuvaana na Simba April 30
"Hii ni kama nusu fainali au fainali nimeangalia rekodi zimenishtua nimeona Yanga haijawahi kushinda au kufungwa na Namungo katika ligi, hii inaleta tafsiri ni mechi kubwa kuliko ya Simba" alisema Nabi
"Tumeanza maandalizi nimewaambia wachezaji wanatakiwa kujiandaa vyema kuhakikisha tunafuta matokeo haya, tuliona ugumu ambao tulikutana nao katika mechi zilizopita ni wakati wa kubadilisha mambo," alisema Nabi
Takwimu zinaonyesha Yanga na Namungo zimetoka sare katika michezo yote ya ligi kuu, Yanga imewahi kuifunga Namungo wakati ikiwa daraja la kwanza katika mchezo wa kombe la FA