Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema wanaendelea vyema na maandalizi kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc ambao utapigwa Jumamosi, April 23 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Bumbuli amesema Yanga imedhamiria kushinda mchezo huo na kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi lengo likiwa kutwaa ubingwa wakiwa na mechi sita mkononi
Bumbuli amesema baadhi ya wachezaji waliokuwa majeruhi wamerejea kikosini baada ya kupona
"Khalid Aucho amerejea, Chico Ushindi amerejea, Yacouba Songne atarejea wakati wowote baada ya kukamilisha mazoezi ya fitnes. Mchezaji pekee ambaye anaweza kukosekana ni Feisal Salum kwani licha ya kuanza mazoezi, taarifa za kitabibu zinataka apumzike zaidi ili apone majeraha vizuri"
"Wanayanga waje kwa wingi uwanjani Jumamosi kuishangilia timu yao, tumedhamiria kuibuka na ushindi," alisema Bumbuli
Tangu Namungo Fc wapande ligi kuu, Yanga haijawahi kupata ushindi dhidi yao, michezo yote ikimalizika kwa matokeo ya sare
Bumbuli amesema wamedhamiria kubadilisha historia hiyo siku ya Jumamosi