Hersi akerwa na wanaozusha kuhusu Aucho

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Apr 2022
Hersi akerwa na wanaozusha kuhusu Aucho

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano Yanga Injinia Hersi Said ameonyesha kukerwa na taarifa za upotoshaji zinazosambazwa na baadhi ya watu katika mitandao ya kijamii kuhusu kiungo Khalid Aucho

Aucho amerejea kikosini hivi karibuni baada ya kuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki tano akiuguza majeraha

Kukosekana kwake kumewapa nafasi baadhi ya watu ambao wamezusha kuwa nyota huyo kutoka Uganda, amegoma kucheza sababu anaidai Yanga

"Aucho ni mchezaji muungwana, ambaye wakati wote anapenda kuwa uwanjani kuipambania klabu. Haidai Yanga hata shilingi moja, kiufupi hakuna mchezaji mwenye madai Yanga"

"Huko tulishapita, sasa hivi tunao wadhamini ambao wanatupa uwezo wa kutimiza mahitaji ya klabu kwa asilimia 100"

"Hizi ni propaganda za 'majitaka' ambazo hazina afya, niwaombe Wanayanga wasiyumbishwe na taarifa hizi za upotoshaji, waendelee kuiunga mkono timu yao kuhakikisha tunatimiza malengo yetu msimu huu"

"Aucho amepona na tayari amerejea kikosini pengine mwishoni mwa wiki tunaweza kumshuhudia uwanjani kutegemea na utayari wake na mahitaji ya Mwalimu katika mchezo dhidi ya Namungo Fc," alisema Hersi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’