Kocha Mkuu wa Ihefu FC, Salhina Mjengwa amesema Yanga wasitarajie mteremko watakapokutana nao kesho kwani wamejipanga kufanya vizuri na kusonga mbele katika raundi inayofuata ya mashindano ya Kombe la Shirikisho (FA).
Ihefu inayoshiriki Ligi daraja la pili Tanzania (SDL) imetinga hatua ya 32 bora baada ya kuitoa Mbeya City.
Hivyo sio timu ya kubezwa.
Mjengwa amesema ingawa wanashiriki SDL, wana uwezo wa kushinda na kusonga mbele.
"Ni kweli hatuna jina lakini tutavuma mara baada ya kuwalaza Yanga na viatu, maana hizi timu kongwe zimezidi dharau na kejeli kwa timu ndogo bila kuangalia kuwa aliyejipanga ndiye anayeibuka ndani ya dakika 90 za mchezo."
"Hatujalala juu ya hili, tumejipanga kisawasawa kuhakikisha kwamba tunafanya vizuri FA pamoja na mwendelezo wa SDL".
Mchezaji huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar alitumia usemi wa 'siku zote unapomuuwa nyani usimwangalie usoni' na kwamba hicho ndiyo wanachokisubiri kuwafanyia Yanga
Kikosi cha Yanga tayari kiko mkoani Mbeya kwa ajili ya mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkali.
Yanga imedhamiria kufanya vizuri kwenye michuano hiyo ikiwezekana kutwaa ubingwa ili kujihakikishia nafasi ya kushiriki michuano ya Kimataifa hata kama ikitokea imeshindwa kutetea ubingwa wake.

ADVERTISE HERE