Nabi kuongeza watano kuunda kikosi cha ubingwa Afrika

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Apr 2022
Nabi kuongeza watano kuunda kikosi cha ubingwa Afrika

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema ili timu hiyo iweze kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa, wanalazimika kuongeza baadhi ya wachezaji kwenye nafasi za ushambuliaji na ulinzi.

Yanga inapewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, hivyo mwakani italiwakalisha taifa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kocha huyo mwenye uraia wa pacha wa nchi za Tunisia na Ubelgiji, amesema anayafuatilia kwa karibu mashindano hayo na amegundua yanahitaji timu yenye wachezaji wenye uzoefu na wapambanaji, hivyo lazima waingie sokoni ili kufanya usajili mzuri

"Timu tuliyonayo msimu huu ni nzuri isipokuwa tunahitaji kwa malengo tuliyonayo kwenye michuano ya kimataifa lazima tuziboreshe baadhi ya sehemu ili kujenga kikosi cha ushindani kwa ajili ya michuano ya kimataifa,"; Nabi amenukuliwa na gazeti la Serikali, HabariLEO

Kocha huyo alisema malengo yao ni kuongeza wachezaji watano, kati yao watatu wa kigeni na wawili wazawa na ana amini kikosi chake kitakuwa tayari kwa mapambano ya kuwania taji la Afrika

Aidha, kocha huyo alisema maandalizi ya timu yake kuelekea mchezo dhidi ya Namungo FC Aprili 23 yanakwenda vizuri na wachezaji wote wapo fiti kwa ajili ya mchezo huo.

Alisema malengo yao ni kuchukua pointi tatu kwenye mchezo huo ili waende kwenye mchezo dhidi ya Simba wakiwa na pengo kubwa la pointi dhidi yao ambao wanashika nafasi ya pili.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
2h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
7h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
11h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
12h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
12h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
16h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’