Yanga kuongeza ushirikiano na klabu nyingine Afrika Mashariki

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Apr 2022
Yanga kuongeza ushirikiano na klabu nyingine Afrika Mashariki

Juzi Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Injinia Hersi Said akiwa na Kocha Msaidizi Cedric Kaze walionekana huko Rwanda wakishuhudia moja ya mechi za ligi kuu iliyoihusisha klabu ya Kiyovu Sport

Jambo lililozungumzwa zaidi ni tetesi zinazowahusisha nyota wa Kiyovu Sport viungo Abeid Bigirimana na Ismail Pitchou wanaotajwa kuwaniwa na Yanga

Hata hivyo hilo sio jambo pekee lililompeleka Injinia Hersi Rwanda kwani amekuwa na mazungumzo na klabu kadhaa ambazo Yanga inakusudia kushirikiana nazo

Ikumbukwe Yanga imefanya Mabadiliko ya mfumo wake wa uendeshaji, Mabadiliko ambayo yamegharamiwa na GSM kwa asilimia 100

Zipo klabu ambazo zimevutiwa na mchakato huo na zingependa kushirikiana na Yanga kuona zinaweza kufanikiwa vipi

Pamoja na kufanya mazungumzo na Kiyovu Sport, Injinia Hersi pia alifanya mazungumzo na klabu ya Rayon Sport ya hukohuko Rwanda

Kwa sasa katika ukanda wa Afrika Mashariki Yanga inatizamwa kama klabu ya mfano, klabu nyingine zikitamani kujifunza kutoka kwao

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
22h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’