Kadi nyekundu yamtesa Nabi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Apr 2022
Kadi nyekundu yamtesa Nabi

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi hana raha kutokana na kupewa kadi nyekundu inayomfanya akose mechi tatu ikiwamo dhidi ya Simba na kasema hajui kilichomfanya mwamuzi Raphael Ikambi kumpa.

Mwamuzi huyo alimlima Nabi dakika za lala salama za mechi ya robo fainali ya Kombe la ASFC dhidi ya Geita Gold kwa ushauri wa mwamuzi wa akiba, Heri Sasii na kocha huyo alisema tangu aanze kufundisha soka Ikambi amemtibulia rekodi yake.

Nabi alisema hakuna mwamuzi aliyewahi kumtolea lugha chafu tangu aanze kufundisha soka na hata hapa nchini licha ya kukutana na uamuzi uliomshangaza.

Alisema alimfuata Sasii kumuuliza juu ya mchezo kumalizika mapema hali ya kuwa kuliongezwa dakika tano za nyongeza, huku ndani yake muda mrefu ukitumika kumtibu beki wa Geita aliyeumia dakika za mwisho.

"Sijajua kipi nilimkosea, nimekuwa nikijiuliza sipati jibu. Sina rekodi ya kuwatusi waamuzi tangu nimefika hapa, kumekuwa kukitokea uamuzi wenye utata lakini sijawahi kufanya vitu vya hovyo," alisema Nabi.

"Nilimfuata mwamuzi wa akiba (Sasii) nikamuuliza imekuwaje dakika zilionyeshwa tano na tumetumia kama tatu pekee? Sijui hapa alikasirishwa na kipi wakati kila mtu aliona jinsi mchezo uliposimama yule mchezaji wao (Geita Gold) alipokuwa anatibiwa"

Akizungumzia mabadiliko ya ratiba, Nabi alisema hatua hiyo ni nzuri kwa kikosi chake ambapo itakwenda kuwapa nguvu ya kimaandalizi kuelekea mchezo wa Simba utakaopigwa Aprili 30.

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
2h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’