Ushindi ni mchezaji hatari anayeandamwa na majeraha

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Apr 2022
Ushindi ni mchezaji hatari anayeandamwa na majeraha

Mtaalam wa viungo klabu ya Yanga Helmy Gueldich amesema mshambuliaji Chico Ushindi atakapokuwa timamu kwa asilimia 100 atawashangaza wengi

Helmy amesema ushindi ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa lakini bado hajaweza kukionyesha tangu alipojiunga na Yanga kutokana na majeraha yanayomsumbua

Ushindi alisajiliwa na Yanga katika usajili wa dirisha dogo mwezi Januari 2022 akitokea klabu ya TP Mazembe wakati kiungo Mukoko Tonombe akijiunga na TP Mazembe

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amewahi kutoa ufafanuzi kwa nini Ushindi hachezi mara kwa mara akitaja sababu ni majeraha ya nyama za paja yanayomsumbua

Ushindi alijiunga na Yanga akiwa na majeraha hayo, baada ya kutibiwa, madaktari walimuandalia program maalum ya mazoezi ili kuhakikisha tatizo lake linapona kabisa

Ushindi ambaye mara kadhaa ameitwa timu ya Taifa ya DR Congo, anafanya mazoezi chini ya uangalizi na karibuni atarejea uwanjani

Tangu ajiunge na Yanga, amecheza mechi mbili za ligi kuu, dhidi ya Mbeya City akiingia kwenye dakika 10 za mwisho na dhidi ya KMC ambapo alianza na kutengeneza bao la pili lililofungwa na Djuma Shabani katika mchezo ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
9h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
17h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’