Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amethibitisha wamepokea barua kutoka Bodi ya ligi kuhusu mabadiliko ya uwanja wa mchezo dhidi ya Ruvu Shooting
Mchezo huo wa ligi kuu ambao awali ulipangwa kupigwa May 04 katika uwanja wa Benjamin Mkapa, sasa umepelekwa mkoani Kigoma na utapigwa katika uwanja wa Lake Tanganyika
Bumbuli amesema Yanga wamepokea taarifa ya mabadiliko hayo na watakwenda mkoani Kigoma huku wakifahamu wao kila uwanja ni nyumbani
ADVERTISE HERE