Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, ameweka wazi kuwa licha ya mwenendo mzuri walionao msimu huu, bado haridhishwi na kiwango cha umakini wa kutumia nafasi za kufunga kwa safu yake ya ushambuliaji
Nabi amesema timu yake imekuwa ikitengeneza nafasi nyingi lakini washambuliaji wake hawajawa makini kuweza kuzitumia nafasi hizo kwa usahihi
"Tumekuwa na wakati mzuri katika michezo mingi msimu huu, lakini mara kadhaa nimekuwa nikiongea kuhusu suala la changamoto ya kutumia nafasi nyingi ambazo tunazitengeneza"
"Mfano kwenye mchezo dhidi ya Azam Fc na hata ule tuliocheza dhidi ya Geita Gold, tuliendelea kuwa na baadhi ya makosa hususani katika suala la kutumia nafasi na kufunga mabao, nadhani bado tuna kazi ya kufanya," alisema Nabi
Yanga imerejea mazoezini kujiandaa na mchezo unaofuata kwenye ligi dhidi ya Namungo Fc ambao utapigwa Jumamosi, April 23 katika uwanja wa Benjamin Mkapa