Kiungo wa Yanga Mzimbabwe, Thabani Kamusoko amekuwa nje ya uwanja kwa muda akiuguza majeraha ya goti, jambo lililomfanya awe kibonge kwelikweli.
Kamusoko ameanza mazoezi na wenzake, ingawa anafanya taratibu ili kurudi katika ubora wake, lakini mwonekano wake wa sasa ni tofauri kwani ameongezeka mwili
Akizungumzia ongezeko hilo la mwili, Daktari wa Yanga, Edward Bavu alisema huwa inatokea kwa mchezaji, ambaye hajafanya mazoezi kwa muda mrefu huku akila vizuri, hivyo Kamusoko sio wa kwanza.
Alisema wameanza kumpa ratiba maalumu ya mazoezi ya kuounguza mwili ili kurudisha utimamu wake wa mwili ili arudi uwanjani mapema.
“Kitaalamu inaweza kutokea, lakini kiuchezaji ule si mwili mzuri. Nimepa ratiba binafsi ya mazoezi na nina imani siku si nyingi atarudi katika mwili wake wa kawaida na kurudi katika kiwango chake kwa haraka,†alisema.
Mwanaspoti

ADVERTISE HERE