Saido kuongoza mapambano mechi zilizobaki

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Apr 2022
Saido kuongoza mapambano mechi zilizobaki

Akiwa ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu mwezi February 2022, mshambuliaji Saido Ntibazonkiza amesema tuzo hiyo imemuongezea mzuka na atahakikisha anapambana katika michezo iliyosalia kuisaidia Yanga kutimiza malengo yake

Saido alianza msimu huu taratibu lakini baada ya kuaminiwa na Kocha Nasreddine Nabi kufuatia majeraha ya Yacouba Songne, mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Burundi amekuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha kwanza akifunga na kutoa pasi za mabao

Saido amefunga mabao sita kwenye ligi na kutoa pasi tano za mabao katika mashindano yote

Katika mchezo uliopita wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc, Saido alisababisha mkwaju wa penati ulioirejesha Yanga mchezoni na baadae kushinda kwa mabao 2-1

"Hii tuzo imenipa hamasa kubwa ya kujituma zaidi katika mechi zilizobaki, kwani najiona nina deni kubwa. Wachezaji wote tunapaswa kupambana kuhakikisha tunatwaa ubingwa. Tuzo hii itarudi tena Jangwani kabla ya msimu kumalizika," alisema Saido

Wachezaji watatu wa Yanga Saido, Feisal Salum na Fiston Mayele wameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi msimu huu wakati kocha Nasreddine Nabi ameshinda tuzo ya kocha bora wa mwezi mara mbili katika msimu huu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’