Yanga, Azam FC zahamishia makali kombe la FA

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Jan 2018
Yanga, Azam FC zahamishia makali kombe la FA
Kufuatia kukamilishwa kwa mechi za duru la kwanza la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kalenda ya soka ya Tanzania sasa inahamia kwenye michuano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), ijulikanayo kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) kwa mechi ya hatua ya 32 Bora katikati ya wiki.

Vigogo Azam FC na Yanga SC wote wanasafiri kwenda mikoani kumenyana na timu za Ihefu FC na Shupavu FC katika hatua ya 32 Bora ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC).

Yanga SC wanakwenda Mbeya kuifuata Ihefu, mechi itakayopigwa Uwanja wa Sokoine mjini humo, wakati Azam FC watakwenda Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro kumenyana na Shupavu FC

Green Warriors iliyowatoa mabingwa watetezi, Simba SC itaendelea kucheza nyumbani mjini Dar es Salaam itakapowakaribisha Singida United Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Uwanja wa Ilulu mkoani Lindi utahodhi mechi mbili mfululizo za wenyeji, Kariakoo United dhidi ya washindi wa pili wa msimu uliopita, Mbao FC ya Mwanza na Maji Maji Rangers dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro.

Maji Maji wataikaribisha Ruvu Shooting Uwanja wa Maji Maji mjini Songea, Njombe Mji FC wataikaribisha Rhino Rangers Uwanja wa Saba Saba mjini Njombe, Kiluvia United wataikaribisha JKT Oljoro Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani na Ndanda FC watakuwa wenyeji wa Biashara United ya Mara Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.

Mechi nyingine; Pamba SC wataikaribisha Stand United Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, Polisi Tanzania watakuwa wenyeji wa Friends Rangers Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, JKT Tanzania watakuwa wenyeji wa Polisi Dar es Salaam na Mwadui FC wataikaribisha Dodoma FC Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga.

Tanzania Prisons wataikaribisha Burkina Faso Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya wakati Kagera Sugar watakuwa wenyeji wa Buseresere FC Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Mchezo kati ya KMC ya kocha Freddy Felix Minziro wa Toto Africans ya Mwanza Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam umeahirishwa hadi Februari 7 wakati mechi nyingine zote zinatarajiwa kucheza siku mbili mfululizo, Januari 31 na Februari 1, mwaka huu.

MECHI ZOTE HATUA YA 32 BORA
Maji Maji v Ruvu Shooting
Njombe Mji v Rhino Rangers
Kiluvia Utd v JKT Oljoro
Ndanda Fc v Biashara United
Pamba SC v Stand United
Polisi TZ v Friends Rangers
JKT Tanzania v Polisi Dar
KMC V Toto Africans (Imeahirishwa)
Ihefu FC v Yanga SC
Mwadui FC v Dodoma FC
Green Warriors v Singida United
Tanzania Prisons v Burkina Faso
Kariakoo United v Mbao FC
Maji Maji Rangers Lindi v Mtibwa Sugar
Kagera Sugar v Buseresere FC
Shupavu FC v Azam FC

BIN ZUBEIRY
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
3h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’