Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi ataukosa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba ambao utapigwa April 30 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Nabi alionyeshwa kadi nyekundu jana kwenye mchezo wa robo fainali kombe la FA dhidi ya Geita Gold baada ya kumlalamikia mwamuzi kutokana na matukio yaliyojitokeza katika mchezo huo
Kwa kuwa michuano ya kombe la FA kanuni zinazotumika ni zilezile zinazotumika kwenye ligi, Nabi atakosa michezo mitatu akianza na mchezo dhidi ya Simba
Nabi atakosekana kwenye benchi tu wakati wa mchezo lakini ataendelea na majukumu yake mengine kama kawaida
Kocha Msaidizi Cedric Kaze ndiye atakayesimama kwenye benchi katika michezo hiyo mitatu
ADVERTISE HERE