Beki Kelvin Yondani ni miongoni mwa wachezaji waliojijengea heshima kubwa wakati wakiitumikia klabu ya Yanga
Ameichezea Yanga kwa zaidi ya miaka 10 na mashabiki walikuwa wakimpa heshima ya kipekee
Tukio alilofanya katika mchezo wa jana kwa kumkanyaga Fiston Mayele kwa makusudi, limeishusha heshima yake
Lakini pia tukio hilo lilihatarisha afya ya mchezaji mwenzake kwani angeweza kumuumiza
Naamini mamlaka za usimamizi wa soka zimeona tukio hili
ADVERTISE HERE