Yanga imetinga nusu fainali ya kombe la FA kwa ushindi wa mikwaju ya penati 7-6 baada ya matokeo ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Geita Gold
Ulikuwa mchezo mgumu ambao matokeo yake yaliamuliwa kwenye dakika za lala salama
Geita Gold walianza kufunga bao la kuongoza kwenye dakika ya 88 lakini mkwaju wa penati katika dakika za majeruhi uliirejesha Yanga mchezoni baada ya mlinzi wa Geita kushika katika eneo la hatari
Djuma Shabani ndiye aliyeweka mpira huo kimiani
Pamoja na kukosa mkwaju wa penati, Djigui Diarra ndiye aliyeipeleka Yanga hatua ya nusu fainali

ADVERTISE HERE