Mzunguuko wa kwanza VPL umekamilika

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Jan 2018
Mzunguuko wa kwanza VPL umekamilika
Leo imepigwa michezo miwili kukamilisha michezo 15 ya mzunguuko wa kwanza ligi kuu ya Vodacom.

Simba imefanikiwa kuwa timu pekee iliyokamilisha mzunguuko wa kwanza bila kupoteza mchezo baada ya leo kuichapa Majimaji FC mabao 4-0.

Singida United nayo imemaliza kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Prisons.



Simba inaongoza ligi ikiwa na alama 35, ikifuatiwa na Azam FC yenye alama 30.

Yanga iko nafasi ya tatu ikiwa na alama 28 kama inavyoonekana kwenye msimamo hapo juu.

Mzunguuko huu umekuwa mgumu sana kwa Yanga kutokana na uhaba wa mabao. Sababu ya hili inafahamika, Yanga imewakosa washambuliaji wake tegemeo kutokana na majeruhi.

Tambwe na Ngoma, wamekosekana kwa muda mrefe wakati Chirwa nae amekuwa akikosekana mara kwa mara.

Simba imefunga mabao 35 kwenye mzunguuko wa kwanza, wakati Yanga imekuwa chini ya kiwango kabisa kwa kufunga mabao 20 pekee.

Wakati Simba ikiwa na tofauri ya mabao (GD) +29, Yanga ina GD +12 pekee.

Hii tayari ni dalili mbaya katika kutetea ubingwa wake kwani upo uwezekano mkubwa bingwa akaamuliwa kwa tofauti ya mabao kutokana na ushindani uliopo.

Kwenye mzunguuko wa pili Yanga inahitaji kuwa na washambuliaji wake wote na italazimika kushinda michezo kwa mabao mengi kuifikia Simba ambayo sasa inaongoza kwa tofauti ya alama saba na mabao 17 dhidi ya Yanga.

Aidha kwa mazingira haya ni muhimu Yanga ikaweka mkazo kwa michuano ya kombe la FA pia.

Yanga inalazimika kuhakikisha inafika fainali ya michuano hiyo kutwaa taji hilo ili kujihakikishia inapata nafasi ya kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao hata kama itakosa ubingwa wa VPL
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
6h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
6h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
19h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1d ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’