Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema Yanga 'imechana mikeka' ya wale wote waliokuwa wakiitabiria kupoteza katika miongoni mwa mechi zake
Ushindi wa mabao 2-1 walioupata ugenini dhidi ya Azam Fc jana, umewafanya Yanga washinde mechi sita zilizopita wakizifunga Biashara United, Mtibwa Sugar, Kagera Sugar, Geita Gold, KMC na Azam Fc
"Tumepata ushindi muhimu ambao unafanya gap la pointi linaendelea kuwa kubwa, sawa nao wana mechi zao watacheza lakini gap la pointi nane litaendelea kubakia vilevile"
"Walihesabu mechi nne, mbili tumepangua inayofuata ni ya kwao kwa hiyo tunawaambia watie nia kwani wanaofuata ni wao," alitamba Bumbuli
Mchezo unaofuata kwenye ligi ni dhidi ya Simba, utapigwa April 30 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Yanga itashuka tena dimbani April 10 katika mchezo wa robo fainali kombe la FA dhidi ya Geita Gold