Naiona Yanga ikienda kufanya vizuri ligi ya mabingwa

Muungwana wa Yanga By Muungwana wa Yanga
β€’
28 Jan 2018
Naiona Yanga ikienda kufanya vizuri ligi ya mabingwa
Mwenendo wa Yanga kwenye ligi umewafanya wengi wadhanie huenda timu isifanye vizuri kwenye michuano ya ligi ya mabingwa inayotarajiwa kuanza Februari 10 ikiivaa St Luis kwenye mchezo wa hatua ya awali.

Hata hivyo hali hiyo ni kawaida kutokea kwa timu yoyote duniani. Wakati mwingine hutokea kwa muda tu.

Kutwaa ubingwa kwa misimu mitatu mfululizo sio jambo jepesi. Hali hiyo inaifanya kila timu inayokumbana na Yanga katika ligi ikamie kusaka heshima ya kuwafunga mabingwa wa kihistoria.

Lakini katika upande mwingine, hakuna shaka kikosi cha Yanga kimeendelea kuimarika na kubadilika kwenye kila mechi.

Ni Yanga hii hii iliyoingia kinyonge kwenye mchezo wa ufunguzi wa msimu August 23, 2017 dhidi ya Simba katika mchezo wa Ngao ya Jamii wengi wakidhani huenda ungekuwa mchezo mwepesi kwa Simba.

Matokeo yake wengi walishikwa na butwaa kwani Simba ililazimika kusubiri bahati ya matuta kupata ushindi.

Oktoba 28 2017 tena, Yanga ikaiduwaza Simba kwa kuilazimisha sare ya bao 1-1 katika mchezo ambao Yanga ilikosa nafasi za dhahiri kuibuka na ushindi.

Ni Yanga hii hii iliyoenda kushiriki michuano ya kombe la mapinduzi ikiwa na 'yoso' wengi lakini ikafanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ambapo ilitolewa kwa bahati ya mikwaju ya penati na URA.

Ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Azam FC umedhihirisha uimara wa kikosi cha Yanga. Ni matokeo mengine ambayo hayakutarajiwa na wengi.

Aidha, ushindi huo umeongeza morali na kujiamini kwa kikosi cha Yanga kuelekea michuano ya klabu bingwa.

Ukifuatilia vizuri rekodi za kocha wa Yanga George Lwandamina utashikwa na butwaa.

Kabla hajaifikisha ZESCO hatua ya nusu fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa misimu miwili iliyopita, timu hiyo ilikuwa ya kawaida sana.

Ni mbinu zake hizihizi ambazo wakati mwingine zinaonekana kuwaboa baadhi ya mashabiki zilifanikiwa akiwa ZESCO.

Si ajabu kuiona timu yake hiyo ya zamani ikijaribu bila mafanikio kumrejesha wakati alipokwenda Zambia kwa ajili ya mapumziko na kisha kupata msiba kwa kufiwa na mwanawe.

ZESCO wametwaa ubingwa wa Zambia msimu huu hivyo watashiriki michuano ya ligi ya mabingwa wao wakianza na JKU ya Zanzibar.

Naamini Yanga itafanikiwa kuvuka hatua ya awali na pia itaweza kutinga hatua ya makundi, muhimu ni kuhakikisha wachezaji muhimu hawakosekani katika michezo minne(miwili nyumbani na ugenini) kuelekea hatua ya makundi.

Kikosi cha Yanga kilichoivaa Azam FC jana ndio kikosi bora kwa sasa. Kama sikosei ni kikosi hicho hicho ukimtoa Kessy, kilitoka sare ya bao 1-1 na Simba, Oktoba 28 mwaka jana.

Kama wachezaji wa kikosi hicho watakuwa fiti, Yanga haina haja ya kuwafikiria wagonjwa kama akina Tambwe, Kamusoko na Ngoma ambao msimu huu afya zao zinasumbua sana.

Ikumbukwe pia Yanga ina hazina ya wachezaji wengi vijana ambao wana kawaida ya kufanya vizuri kila wanapopata nafasi.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’