Yanga hii kinatoka chuma, kinaingia chuma

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Apr 2022
Yanga hii kinatoka chuma, kinaingia chuma

Jambo la kujivunia katika kikosi cha Yanga msimu huu, ni timu kutotegemea mchezaji mmoja katika kupata matokeo

Mashabiki wanayo haki ya kuhoji kwa nini majeruhi ni changamoto kubwa kwa timu yao, lakini pia wanapaswa kupongeza kazi kubwa iliyofanywa na benchi la ufundi kuwafanya wachezaji wote kuwa tayari kuipigania timu pale wanapopewa nafasi

Kumekuwa na mabadiliko ya kikosi kutoka mchezo mmoja hadi mwingine lakini Wananchi wameendelea kupambana na kupata matokeo

Leo Yanga itashuka uwanja wa Azam Complex kuikabili Azam Fc katika mchezo muhimu wa ligi kuu

Jana Kocha Msaidizi Cedric Kaze alithibitisha kuwa Feisal Salum na Khalid Aucho hawatakuwa sehemu ya mchezo huo kutokana na changamoto ya majeruhi inayowakabili

Hii ina maana katika nafasi zao kocha Nasreddine Nabi ataweka wachezaji wengine, Saido Ntibazonkiza akitarajiwa kurejea kikosini baada ya kupona majeraha na Salum Abubakar 'Sure Boy' ambaye anatimiza vyema majukumu ambayo huwa yanafanywa na Aucho

Farid Mussa katika mechi za karibuni ametumika kama mlinzi wa kushoto, anaweza kukosekana leo baada ya kuugua lakini jambo jema ni kuwa Yassin Mustafa, David Bryson na Kibwana Shomari wote wamerejea

Kaze pia alidokeza kuwa yawezekana Yannick Bangala leo atakosekana baada ya kuumia mazoezini hatma yake ilitegemea mazoezi jana

Kama atakosekana, inaweza kuwa nafasi kwa Zawadi Mauya kurejea kwenye kikosi cha kwanza akicheza sambamba na Sure Boy

Winga Jesus Moloko nae amepona na kurejea mazoezini, kama benchi la ufundi litajiridhisha na utayari wake, anaweza kutumika leo

Mabadiliko makubwa yanatarajiwa kwenye eneo la kiungo tu kwani safu ya ulinzi na ushambuliaji hakuna changamoto kubwa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
19h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
23h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’