Nabi anawania rekodi ya aina yake leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Apr 2022
Nabi anawania rekodi ya aina yake leo

April 23 2021 uwanja wa Benjamin Mkapa ulipigwa mchezo wa duru ya pili ligi kuu ya Tanzania bara kati ya Yanga dhidi ya Azam Fc, mchezo huo ukimalizika kwa Azam Fc kuibuka na ushindi wa bao 1-0

Ulikuwa mchezo wa kwanza kwa kocha mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi ambaye ndio kwanza alikuwa amesaini mkataba na Wananchi

Huo ndio mchezo pekee ambao Nabi amepoteza kwenye ligi kuu tangu alipojiunga na Yanga

Kama leo Yanga itaibuka na ushindi dhidi ya Azam Fc au hata kutoka sare, Nabi ataweka rekodi ya aina yake pamoja na kikosi cha Yanga

Wananchi watakuwa wamedumu zaidi ya siku 360 pasipo kupoteza mchezo kwenye ligi. Baada ya mchezo wa leo, mchezo utakaofuata ligi kuu ni dhidi ya Simba utapigwa April 30

Leo Yanga haisaki ushindi tu, bali inawania rekodi ya aina yake ambayo kwa hakika inadhihirisha ni kwa kiasi gani Wananchi wamedhamiria msimu huu

Yanga ni klabu pekee ambayo haijapoteza mchezo katika msimu huu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
13h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
17h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
21h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
22h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’