Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi, amesema ameuomba uongozi kuwafanyia vipimo upya wachezaji wake Feisal Salum na Khalid Aucho ili kujiridhisha na ukubwa wa tatizo lao.
Feisal anasumbuliwa na misuli ya nyama za paja aliyoyapata tangu Januari mwaka huu huku Aucho akijitonesha goti akiwa kwenye kambi ya timu ya taifa lake ya Uganda, Cranes.
Nabi amesema ni pigo kuwapoteza wachezaji hao akiwa katikati ya kampeni ya kuwania ubingwa wa ligi kuu msimu huu
"Haiingi akilini kuwapoteza wachezaji wako muhimu kwa wakati mmoja tena katika kipindi muhimu kama hiki nimeiagiza timu yetu ya madaktari kuwafanyia upya vipimo ili kujua ukubwa wa majeruhi yao," alisema Nabi
Nabi amesema pamoja na upana wa kikosi cjake, lakini inapendeza kipindi kama hiki wachezaji wake wote wanakuwa fiti kwa ajili ya kupambania malengo yao
Kikosi cha Yanga tayari kimeingia kambini kujiandaa na mchezo dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa April 06 katika uwanja wa Azam Complex
Yanga inakabiliwa na michezo miwili inayofuatana kwani baada ya kuikabili Azam Fc April 06, watapumzika siku nne tu kisha kushuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Geita Gold katika mchezo wa robo fainali kombe la FA