Ni siku 60 za jasho na damu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Apr 2022
Ni siku 60 za jasho na damu

Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze amesema kikosi chake kinaingia katika miezi miwili migumu lakini wamejipanga kupambana kuhakikisha wanafikia malengo ya kushinda mechi zote ili kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu, Tanzania Bara na Kombe la FA msimu huu

Kaze alisema timu yao itakuwa na ratiba ngumu kwa mwezi huu na ujao na hiyo ndio fainali yao na kuhakikisha wanapata matokeo chanya katika michezo yote wakianzia mechi dhidi ya Azam FC itakayochezwa Jumatano ijayo.

Kocha huyo alisema mara kadhaa amekuwa akiwasisitiza wachezaji kuongeza umakini na kujifunza mbinu mpya ili kuhakikisha wanafanikiwa katika malengo waliyonayo ya kushinda michezo yote iliyoko mbele yao.

"Hii miezi miwili ya fainali kwetu kwa sababu tunahitaji kupambana kushinda mechi zote zilizopo mbele yetu, tunacheza na Azam FC halafu mechi ya FA (dhidi ya Geita), kabla ya Simba hizo zote ni mechi za muhimu kwenye makombe mawili tofauti," alisema Kaze.

Alisema kiufundi mechi chache lakini ni ngumu na zilizo muhimu kupata matokeo chanya wakati msimu ukielekea tamati.

"Mei ni mwezi wa kumalizia kila kitu, sasa unaweza kuona jinsi ratiba ilivyo na umuhimu, tunahitaji kufanya mazoezi ya pamoja kwa muda mrefu na kupata mechi za kirafiki, kujiweka sawa katika kufikia malengo yetu"

Aliongeza mchezo dhidi ya Azam FC ni mechi muhimu na inayotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa lakini dhamira yao ni kuhakikisha wanapata pointi tatu.

Mrundi huyo pia alisema tayari ameanza kutengeneza mfumo mwingine wa uchezaji ambao utawasaidia wakikutana na mechi ngumu, au kwenye viwanja vya mikoani ambavyo si rafiki.

"Tumejipanga kuhakikisha timu inakuwa na mifumo mbalimbali ya uchezaji na si kutegemea mfumo mmoja ambao siku ukitakaa, au ukikuta uwanja hauruhusu, au wapinzani kukudhibiti, basi timu inakosa njia nyingine ya kufanya," alisema Kaze.

Mrundi huyo aliongeza katika mechi ya kirafiki dhidi ya Mafunzo iliyochezwa Jumatano iliyopita kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, kuna wakati alichezesha mastraika wawili mbele, Fiston Mayele na Heritier Makambo, wakiwa na mfumo wa 4-4-2, lengo ikiwa ni kutazama mfumo mwingine, hasa pacha ya wachezaji hao wawili mbele, ambao anaamini baadaye unaweza kuwasaidia.

"Tulianza na mfumo tuliozoea, lakini baadaye tukachezesha mastraika wawili mbele, hiyo ni kutaka kujaribu aina nyingine ya mfumo, maana kuna siku tutataka kutumia mastraika wawili, kama siku hiyo mechi itakuwa ngumu, matokeo mazuri hajayapatikana, au kwenye viwanja vigumu, sasa tunaona kama tunaweza kuwatumia Mayele na Makambo wote kwa pamoja ili wakae pale mbele, wawape presha mabeki, mawinga nao wawe wanakwenda pembeni na kupiga krosi nyingi," Kaze alisema.

Yanga yenye pointi 48, ndio timu pekee mpaka sasa haijapoteza mechi yoyote kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa inaongoza katika msimamo baada ya kushinda mechi 15 na sare michezo mitatu.

Kikosi cha Yanga kiliingia kambini jana rasmi kuanza maandalizi ya kuwakabili Azam FC

IPP Media

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
2h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
7h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
11h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
12h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
12h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
17h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’