Vinara wa ligi kuu ya NBC Yanga mwezi huu wanaweza kujiweka katika nafasi nzuri katika mbio za ubingwa wa ligi kuu pamoja na michuano ya kombe la FA
Katika mwezi huu wa April, michezo miwili muhimu ya ligi kuu dhidi ya Azam Fc na Simba itapigwa pamoja na mchezo wa robo fainali kombe la FA dhidi ya Geita Gold
April 06 Wananchi watashuka uwanja wa Azam Complex kuikabili Azam Fc katika mchezo ambao ushindi utazidi kuiweka Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama 14 dhidi ya Simba ambayo itashuka dimbani April 07 kule Mkwakwani kucheza na Coastal Union
April 10 Yanga itakuwa uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Geita Gold katika mchezo wa robo fainali kombe la FA. Ushindi utawahakikishia Wananchi kutinga nusu fainali na pengine watakutana na watani zao Simba katika hatua hiyo kama Simba watashinda mchezo dhidi ya Pamba Fc April 13
April 30 Wananchi watakamilisha mwezi April kwa mchezo dhidi ya watani zao Simba, mchezo ambao unaweza kutoa taswira ya ubingwa msimu huu
Kama Yanga itashinda mchezo huu ni wazi, utahitajika muujiza kwenye soka kuwanyima ubingwa msimu huu
