Yanga yataka ufafanuzi majeraha ya Fei Toto

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
31 Mar 2022
Yanga yataka ufafanuzi majeraha ya Fei Toto

Klabu ya Yanga imesema inahitaji kupewa ufafanuzi wa kitabibu juu ya jeraha la kiungo wao, Feisal Salum kutoka kwa daktari wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Lisobine Kisongo.

Kauli hiyo inakuja kufuatia Dk Kisongo kutangaza juzi kuwa Feisal ni majeruhi wa muda mrefu ndio maana walimwondoa katika mpango wa kumchezesha katika mechi ya Stars dhidi ya Sudan.

Katika mahojiano na gazeti la HabariLEO, Ofisa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Hassan Bumbuli alisema wanashangazwa na taarifa ya daktari huyo kusema Feisal ni majeruhi na wakati huo huo, walimchezesha katika mechi ya kwanza ya kirafiki kati ya Stars dhidi ya Afrika ya Kati na mchezaji alicheza vizuri

"Tunashangaa kama walijua mchezaji ni majeruhi kwanini walimchezesha tangu awali? Mchezaji ni kweli alikuwa majeruhi na alipata nafuu kwa maana hiyo itakuwa alijitonesha kidonda katika mchezo wa kirafiki wa kwanza wa Stars," alisema

Kwa mujibu wa Dk Kisongo, Feisal ana jeraha kwenye misuli ya paja na kwa hiyo alipumzishwa kucheza mechi dhidi ya Sudan kwa faida yake mwenyewe na timu yake, kwani akiendelea anaweza kutocheza tena kwa kuwa tatizo linakua

Bumbuli amesema Yanga wanasubiri ufafanuzi wa daktari huyo wa kitabibu ndipo wanaweza kuwa na jibu juu ya mchezaji, ambaye tayari hadi anajiunga na Stars alitoka kucheza mechi kadhaa zilizopita za Ligi Kuu, ingawa sio kwa kiwango chake cha awali

Hata hivyo, HabariLEO jana lilimtafuta tena Dk Kisongo kuhusu Yanga kumtaka kutoa ufafanuzi, ambapo alisema kuwa yeye hafanyi siasa ya mpira kwenye afya ya mchezaji, bali anafanya sayansi

Alisema ni kweli mchezaji huyo ni majeruhi na mchezaji mwenyewe pamoja na daktari wa klabu yake wanatambua na kusisitiza kwamba mchezaji ana haki ya kupatiwa matibabu

"Mtafute Feisal mwenyewe anajua ukweli kama yuko tayari kuzungumza hata daktari wa klabu yake anajua, kwa hiyo mimi sifanyi siasa ya mpira kwenye afya ya mchezaji, nasema ukweli na kusimamia sayansi," alisema

Kuumia kwa mchezaji huyo ni pigo kwa Yanga ambao wana mchezo mgumu mbele yao dhidi ya Azam FC Aprili 6, mwaka huu mchezo wa Ligi Kuu unaotarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi

HabariLEO

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’