Aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga Princess Aisha Masaka amejiunga na klabu ya BK Hacken inayoshiriki ligi kuu ya Wanawake, Sweden
Masaka alisafiri jana kwenda Sweden kujiunga na timu hiyo baada ya taratibu zote za usajili wake kukamilika
Leo klabu ya BK Hacken imemtambulisha rasmi Masaka kuwa mchezaji wao
BK Hacken walitwaa ubingwa wa ligi kuu ya Sweden mwaka 2020 pia wakishiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya katika kila msimu huu
Hii ni nafasi kwa Masaka kuitangaza Tanzania na Yanga Princess klabu iliyomlea na kumpa nafasi ya kuonyesha kipaji chake
Kila la kheri katika klabu yake mpya..!
ADVERTISE HERE