Mlinzi wa kulia Paulo Godfrey 'Boxer' ameendelea kuimarika jana akiwa bora sana kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Mafunzo Fc
Baada ya Kibwana Shomari kupata majeraha, Boxer anaonekana yuko tayari kuchuana na Djuma Shabani kuwania nafasi upande wa kulia
Changamoto ambazo anapaswa kuzifanyia kazi ili awe bora zaidi ni katika kufanya maamuzi katika eneo la mwisho na kuboresha krosi zake
Boxer amekuwa mahiri sana katika eneo la ulinzi. Sio mchezaji ambaye anaweza kuzidiwa kasi na mawinga wengi hapa Tanzania
Kibwana amepona lakini ameendelea kurejeshwa kikosini taratibu ili kuhakikisha hatoneshi majeraha baada ya kufanyiwa upasuaji wiki kadhaa zilizopita
ADVERTISE HERE