Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Kim Poulsen amesema kiungo Feisal Salum 'Fei Toto' ameenguliwa katika kikosi cha timu ya Taifa kutokana na majeraha yanayomsumbua
Kesho Jumanne, Tanzania itacheza na Sudan katika mchezo wa Kimataifa wa kirafiki ambao uko kwenye kalenda ya FIFA
Daktari wa timu ya Taifa amesema wamelazimika kumuacha Feisal ili apete muda zaidi wa kutibu majeraha hayo
"Feisal alipata majeraha ya kuchanika msuli wa paja January 26 akiwa na timu yake, katika kipindi chote tangu wakati huo, amekuwa akitibiwa lakini baada ya kumfanyia vipimo tumeona jeraha lake bado halijapona vizuri"
'Tungeweza kuendelea kumtumia lakini kwa maslahi yake, ya klabu na Taifa kwa ujumla tukaona vyema tukamruhusu ili apate muda zaidi ya kutibu jeraha hilo," alisema Daktari wa Stars
Feisal alicheza mchezo uliopita dhidi ya Afrika ya Kati akionyesha kiwango bora katika eneo la kiungo