Jambo moja kubwa ambalo Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amefanikiwa sana msimu huu ni kuunda kikosi kilichotegemea mchezaji mmoja mmoja
Wengi wamekuwa wakijiuliza inakuwaje Yanga hii ambayo kuna wakati inawakosa mpaka wachezaji 11 lakini bado inaendelea kushinda?
Kwa sababu timu sio tegemezi, Nabi ametengeneza mfumo halafu akawaandaa wachezaji wake wote kuwa tayari kutumika katika mfumo huo
Alipoumia Yacouba Songne mwezi Navemba mwaka jana, wapo waliodhani kuwa huo ulikuwa mwanzo wa Yanga kuanguka
Kwani pamoja na kuwa Yacouba hakufunga katika mechi zile za mwanzo alizocheza, alikuwa na mchango mkubwa sana akitoa pasi mbili za mabao katika michezo mitano
Alipoumia nafasi yake akaingia Saido Ntibazonkiza ambaye nae amefunga mabao sita na kutoa pasi tano za mabao ligi kuu na kombe la FA
Nae akapata majeraha, kakosa michezo miwili iliyopita lakini Dickson Ambundo, Chico Ushindi wamefanya vizuri katika nafasi yake
Ushindi alianza kwa mara ya kwanza msimu huu katika mchezo dhidi ya KMC, akatengeneza bao lililofungwa na Djuma Shabani
Jesus Moloko amekosekana kwa takribani michezo minne lakini katika eneo lake Denis Nkane anafanya vizuri
Katika safu ya ulinzi ni Bakari Nondo Mwamnyeto na Yannick Bangala pakee waliocheza mechi nyingi lakini wengine kuna nyakati walikoseka na lakini haikuwa changamoto kwa Yanga
Katika eneo la kiungo Khalid Aucho amekuwa akisumbuliwa na tatizo la misuli, lakini Salum Abubakar 'Sure Boy' amefanya vyema katika nafasi yake
Kuwa na wachezaji wengi wanaocheza nafasi zaidi ya moja pia ni faida nyingine ya Nabi katika kikosi chake
Bangala, Job, Feisal, Farid, Kaseke hawa wote wanaweza kutumika katika nafasi zaidi ya moja kulingana na mahitaji ya timu
Kwa hakika msimu huu Yanga imejipanga kushinda ubingwa, dhamira imeonekana katika mipango na matokeo yanapatikana uwanjani