FT : Azam FC 1-2 Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Jan 2018
FT : Azam FC 1-2 Yanga
Mabingwa watetezi ligi kuu ya Vodacom Yanga leo wamedhihirisha kuwa licha ya changamoto zinazowakabili, wanao uwezo wa kuetetea taji lao kwa msimu wa nne baada ya kuilaza Azam FC mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Azam Complex, Chamazi.

Yanga imekuwa timu ya kwanza kuifunga Azam FC msimu huu tena ikipata ushindi katika dimba lao la nyumbani, sehemu ambayo ni nadra sana kwa Azam FC kupoteza mchezo.

Iliwachukua dakika tatu wenyeji Azam FC kufunga bao la kuongoza kupitia kwa Shabani Iddi aliyewahi mpira dhaifu uliokuwa umeokolewa na Tshishimbi.

Yanga iliuanza taratibu mchezo huo hata hivyo baada ya dakika 15,iliweza kurejea mchezoni na kutawala sehemu ya kiungo.

Raphael Daudi na Papi Tsishimbi waliwapoteza kabisa viungo wa Azam FC ambapo Mwalimu wao alilazimika kumtoa mshambuliaji Author na kumuingiza Hozza ili kwenenda na kasi ya viungo wa Yanga.



Kwenye dakika ya 30, mpira mrefu wa Ibrahim Ajib ulimponyoka mlinda lango wa Azam FC na kuangukia miguuni mwa Obrey Chirwa ambaye bila ya ajizi, aliisawazishia Yanga.

Ikiendelea kutawala sehemu ya kiungo Yanga iliwafanya Azam FC warudi kujilinda ambapo kwenye dakika ya 44, Gadiel Michael Mbaga aliwaadhibu waajiri wake wa zamani kwa bao la shuti kali alilopiga nje ya 18.

Pasi ya kutenga ya Papi Tshishimbi ilitambaa na kujaa kwenye mguu wa kushoto wa Gadiel ambaye shuti lake lilimshinda mlinda lango wa Azam FC.



Kipindi cha pili Azam FC ilijaribu kusaka bao la kusawazisha bila mafanikio kutokana uimara wa safu ya ulinzi wa Yanga.

Aidha, mchezo huo ulishuhudia kadi sita za njano, moja nyekundu kwa Salum Abubakar kwenye dakika ya 81.

Wachezaji wawili wa Yanga walioonyeshwa kadi za njano ni Kelvin Yondani na Papi Tshishimbi.

Juma Mahadhi na Geofrey Mwashiuya waliingia kuchukua nafasi za Ibrahim Ajib na Emanuel Martin aliyepata majeraha kwenye kipindi cha pili.

Matokeo hayo yanaifanya Yanga ipunguze tofauti ya pointi baina yake na Azam FC kuwa mbili baada ya kufikisha alama 28 huku Azam ikisalia nafasi ya pili na alama 30.

Matokeo ya michezo mingine iliyopigwa leo;

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’