Licha ya kuendelea kuimarika baada ya kupata changamoto ya misuli, kiungo wa Yanga Khalid Aucho amejumuishwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Uganda
Leo Uganda ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Tajikistan na kulazimishwa sare ya bao 1-1
Kocha Mkuu wa Uganda Cranes Micho hakumtumia Aucho katika mchezo huo akieleza bado hakuwa timamu kwa asilimia 100 kutokana na matatizo ya misuli yaliyokuwa yakimkabili
Aucho alikosa michezo miwili iliyopita ligi kuu kutokana na changamoto hiyo lakini ni wazi atakuwa tayari kurejea kikosini baada ya kalenda ya Kimataifa
ADVERTISE HERE